HISTORIA YA NENO MARANGU "ENEO LENYE MAJI YENYE MAAJABU"

Kihistoria jina Marangu linatokana na neno Morangu neno la kichaga cha zamani kabla ya kuchakachuliwa na usasa,maana halisi ya neno hili ... thumbnail 1 summary
Kihistoria jina Marangu linatokana na neno Morangu neno la kichaga cha zamani kabla ya kuchakachuliwa na usasa,maana halisi ya neno hili ni nchi yenye maji mengi.

Photo: MARANGU ENEO LENYE MAJI YENYE MAAJABU

Kihistoria jina Marangu linatokana na neno Morangu neno la kichaga cha zamani kabla ya kuchakachuliwa na usasa,maana halisi ya neno hili ni nchi yenye maji mengi.

Kwa wageni wanaofika eneo hili ambalo lipo kwenye mitelemko ya mlima Mashariki kitu cha kwanza kukiona ni msitu mzito wa migomba na miti,cha pili ni madaraja yasio na idadi yanapita  juu ya mito na chemichemi nyingi zilizopo eneo hili ambapo pia ni makao makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.

Moja ya maeneo yenye maajabu ni kijiji cha Ashira ambacho ni  maarufu kutokana na kuwa karibu na Shule ya Sekondari ya Ashira ambayo kwa miaka mingi mamia na mamia ya wataalamu wamepitia hapa.Ndani ya kijiji hiki kuna msitu mkubwa uitwao Yenunyi ambao ni chanzo kikubwa sana cha maji kwani kuna chemichemi nyingi zinazoanzia hapa.Maji ya chemichemi hizi ni meupe na matamu na husambazwa kwa mfumo wa mabomba na mifereji kwenda kwenye taasisi na vijiji vyote vya karibu.

Katikati ya msitu huu ndipo yalipokuwa makazi ya Mkuu wa ukoo wa Mtui aliyeitwa Kimori.Huyu aliishi wakati ule koo mbalimbali zilikuwa zinapigana ilikuweza kupata ukoo wenye nguvu kuunda utawala yaani Umangi.

Hivyo kwa wakati ule kulikuwepo na ushindani mkubwa kati ya ukoo wa Mtui na ule wa Lyimo,kila wakati wa vita watu wa Mshiri walikuwa wanawachukua maiti na majeruhi wao nyumbani na siku ya pili watu hawa walioonekana tena sokoni na mtaani wakiwa wazima kabisaa.

Jambo hili lilitishia usalama wa ukoo wa Lyimo kwani kila mara kutokana na kutoogopa kifo askari wa Mshiri walipigana kwa ari kubwa na kuwashinda wenzao huku wakichukua mifugo na mateka wengi.

Ili kupata siri ya jambo lile,viongozi wa ukoo wa Lyimo walimtuma mwanamke ambaye alijifanya kafukuzwa na mumewe na aliomba hifadhi kwa ukoo wa Mtui.Kwa sababu alikuwa amekwisha fundishwa baada ya kuolewa na mmoja wa watu wa Mtui kama alivyofanya Delila naye alimlaghai mumewe mpaka akatoa siri.

Siri alioitoa ni kuwa Mkuu wa mzee Kimori alifuga Konokono mkubwa aliejulikana kama Kikoru,huyu alikua na uwezo mkubwa wa kuponya majeraha ya askari walioumia na kuwafufua maiti waliofia vitani tu.Alifanya hivyo kwa kulamba miili yao na kila aliepitiwa na konokono huyu alipona jeraha au kufufuka.

Baada ya kupata siri ile askari wa Lyimo walifanya mashambulizi matatu ya nguvu,shambulizi la tatu ndipo jeshi la Lyimo liliwazidi nguvu askari wa wa Mtui mpaka waakamfikia Kikoru.

Walimchoma kwa mikuki mingi na kumuua,kabla ya kufa alilia kwa sauti kubwa ya kutisha iliyosikika eneo lote la Marangu huku akitoa damu nyingi sana.Baadae damu ile iligeuka kuwa maji ambayo mpaka leo inaaminika yanatoka sehemu hiyo.

Baada ya hapo ukoo wa mtui uliwekwa chini ya ukoo wa Lyimo na kuwa mtawala wa eneo lote la Marangu chini ya Mangi aliejulikana kama Kilamia yani Mkandamizaji. 

Kwa msaada wa  Maliasili Zetu