LIFAHAMU PORI LA AKIBA LA SELOUS

Sehemu asilia ya Dunia ambayo Haijaharibiwa. Pori la Akiba la Seous limepata jina lake kutokana na mwindaji na mtaalamu wa mazingira as... thumbnail 1 summary
Photo: PORI LA AKIBA LA SELOUS

Sehemu asilia ya Dunia ambayo Haijaharibiwa.

Pori la Akiba la Seous limepata jina lake kutokana na mwindaji na mtaalamu wa mazingira asilia Friderick courtney Selous aliyefariki mwaka 1917.Selous alizikwa katika pori hili na kaburi lake linaweza kuonekana kwa kufuata barabara ya Beho Beho- Matambwe.

Pori la Akiba Selous ni eneo lililohifadhiwa kisheria,kubwa kuliko yote Duniani,linalofikia kilometa za mraba 50,000.Ni kubwa kuliko eneo la nchi ya Switzerland au Denmark.

Kutokana na upekee wa ikolojia yake muhimu pori hili lilitangazwa na umoja wa Mataifa kuwa Eneo la Urithi wa Dunia mwaka 1982. Kutokana pia na spishis mbali mbali zinazo ishi ndani ya pori hilo zikiongozwa na Tembo wapatao 80,000 ,Nyati 160,000, Viboko 40,000, Simba 5,000 na wanyama wengine wengi.Pia wamo ndege wazuuri sana wapatao spishi 440.

Kutokana na ukubwa wake,umbo la nchi,lina mito na maziwa,nyika za migunga na miombo,mapululu ya wazi,misitu mikubwa inayoambaa na mito,mimea ya ardhioevu pia mito mikubwa unakatiza ndani ya pori hilo kama mto Rufiji,Ziwa Tagalala na maporomoko ya Stieglers ni moja ya vivutio vikubwa vya Pori la Akiba la Selous.

Utalii hususani wa wanyamapori na ndege ni moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya nchi yetu.

TUSHIRIKIANE KUWALINDA WANYAMA NA KUYALINDA MAZINGIRA.Sehemu asilia ya Dunia ambayo Haijaharibiwa.

Chanzo: Maliasili zetu