Watu wawili wakamatwa na meno ya Tembo ya Sh milioni 90

Na   Walter   Mguluchuma   Katavi   Watu wawili     Charles   Gerald    Ngonyani(38) Mkazi wa Kijiji cha Uruwila   Wilaya ya Mlele Mkoa... thumbnail 1 summary
Na  Walter  Mguluchuma  Katavi
 Watu wawili    Charles  Gerald   Ngonyani(38) Mkazi wa Kijiji cha Uruwila  Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi na  Geofrey  Ngonyani (22) Mkazi wa Mkoa wa Mwanza  wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kukamatwa na meno ya Tembo  vipande 20 yenye uzito wa kilo 61 yenye thamani ya Tsh Milioni 90 wakati wakiyasafirisha kwenye basi la Kampuni ya Adventure  Conection
 Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari watuhumiwa hao walikamatwa hapo Oktoba 11 mwaka huu majira ya saa nane na nusu mchana katika eneo la stendi kuu ya mabasi ya Mpanda mjini katika Mtaa wa mji mwema
Alisema watuhumiwa hao walikamatwa  wakiwa wamepakia meno hayo ya Tembo kwenye basi la kampuni ya Adventure Conection lenye Namba za usajiri  T 792 ALF aina ya Scania  lenye makao yake makuu Mkoani Kigoma linalofanya safari zake kutoka Mkoa wa Katavi kwenda Kigoma
Kidavashari alifafanua watuhumiwa hao walikamatwa  na  meno hayo ya Tembo  ambayo walikuwa wameyaficha kwenye  Buti la Basi hilo na mengine  kwenye kelia huku wakiwa wameyahifadhi ndani ya mabeji matano ya salifeti
 Alisema   siku hiyo ya tukio  majira ya saa sita mchana jeshi la polisi  walipata taarifa kutoka kwa raia wema  kuwa kuna watu  watatu watasafirisha meno  ya Tembo  kutoka Mkoani Katavi na kuyasafirisha kuyapeleka Mkoani Kigoma kupitia kampuni ya basi  ya   Adventure Conection
 Alieleza baada ya polisi kuwa wamepata taarifa hizo waliandaa mtego wa kuwakamata watuhumiwa hao katika eneo hilo la stendi ya Mabasi
Alifafanua  watuhumiwa hao walifika kwenye eneo la stendi na kupakia meno hayo ya tembo  kwenye buti la gari  beji tatu za aina ya salifeti na beji mbili nyingine  waliziingiza ndani ya basi kwa kupitia  kwenye dirisha la basi huku muda wote huo polisi wakiwa  kwenye mtego wa kuwakamata
Alisema watuhumiwa hao  walikuwa wakishirikiana na mwenzao mmoja aliye fahamika kwa jina la John Kajuti  ambae alifanikiwa  kutoroka   mara baada ya kuona wenzake wamekamatwa
Jeshi la polisi linaendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo ambae aliyetoroka  ili  aweze kuunganishwa na wenzake kujibu mashitaka yanayo wakabili
Kamanda Kidavashari alisema watuhumiwa hao wawili waliokamatwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani ili waweze kujibu  mashitaka yao ya kupatikana na nyara za Serikali
Mwisho