WANASIASA WATAKIWA KUTOSHIRIKI KATIKA USHAWISHI WA UHARIBIFU WA MISITU NA MAZINGIRA NCHINI

Na Abdulaziz Ahmeid-Dodoma  Wanasiasa wameombwa kutoa ushirikiano kwa taasisi na wadau mbalimbali wanaoshughulika na uhifadhi wa misit... thumbnail 1 summary
Na Abdulaziz Ahmeid-Dodoma 
Wanasiasa wameombwa kutoa ushirikiano kwa taasisi na wadau mbalimbali wanaoshughulika na uhifadhi wa misitu na mazingira badala ya wao kuwa ni miongoni mwa watu ambao wanaoshiriki na kusababisha uharibifu wa mazingira unaondelea kwa kasi hapa nchini. 
Wito huo umetolewa leo mjini Dodoma na mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa jamii wa usimamizi wa misitu Tanzania(MJUMITA)Bi Rahima Njaidi Wakati wa ufunguzi wa warsha na mkutano mkuu wa 14,ambao umeshirikisha wanachama wajumuia hiyo na wadau mbalimbali wanaoshughulika na uhifadhi wa misitu na mazingira toka kanda sita Nchini. 
Bi Njaidi alibainisha kuwa ili kufaniwa katika mapambano na harakati za kuhifadhi misitu na mazingira ni wajibu kwa wanasiasa kushirikiana na taasisi mbalimbali zilizopo katika mapambano na harakati hizo zenye lengo la kuokoa misitu inayoharibiwa kwa kasi nakutishia ‘ kupitia mpango huo Wanajamii wamediriki kuwahoji viongozi wao katika mchakato mzima wa usimamizi endelevu wa rasilimali misitu ambapo suala la Mapato ya vijiji vya uhifadhi ni moja ya changamoto iliyoonekana katika warsha hii’ alibainisha Njaidi 
Akimalizia taarifa yake katika warsha hiyo Njaidi aliviomba vijiji kuachana na baadhi ya wanasiasa ambao kwa kiasi kikubwa wana katika jamii na pia ni washiriki wakubwa uharibifu wa misitu na mazingira kwa kuwaruhusu wananchi wanaowaongoza kuishi na kufanya shughuli za kibinadamu zinazoharibu maliasili kwa lengo la kuwafurahisha wanaowaongoza au kwa maslahi binafsi Nae Bw Musa Mkoyage,
Diwani wa kata ya Likongowele wilayani Liwale aliitaka MJUMITA iwaelimishe wanajamii juu ya ugawanaji wa mapato kama vile ilivyoainishwa katika vijiji vingine ambavyo tayari vimeishaanza kupata faida za misitu huku mapato yote yakibaki kijijini na kuweza kuendeleza shughuli mbali mbali za maendeleo. 
Mkoyage pia alieleza kuwa katika kuokoa misitu inayoharibiwa kwa kasi na kutishia uwepo wake hapa nchini na kusababisha hofu ya nchi kugeuka jangwa Akifungua Warsha hiyo ya siku mbili,Mkuu wa wilaya ya Dodoma,Bw Lefy Gembe kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma,Bi Chiku Galawa Aliwataka wajumbe wa mkutano huo kufanya tathmini ili kujua ni kwa kiasi gani taratibu na kanuni za uvunaji endelevu zinasimamiwa na kufanikiwa ili kila mwananchi ashiriki kulinda na kuhifadhi misitu na mazingira kwa manufaa ya jamii ‘Uvunaji endelevu ni suala la kisheria hivyo ni muhimu kwa wananchi kutekeleza taratibu na sheria zilizopo ili misitu iweze kuwa endelevu na Iwe yenye tija kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo. 
Warsha hiyo ya siku mbili iliyoandaliwa MJUMITA na kushirikisha wadau mbalimbali ikiwemo Jumuiko la maliasili Tanzania(TNRF) ikiwa na lengo kuu la kutafuta mbinu za kupambana na uharibifu wa misitu na mazingira na kufanya usimamizi na uvunaji endelevu
 kutoka kulia ni mkurugenzi wa Mjumita Bi Rahima Njaidi;Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la Mpingo Bw Gasper Makala;mkurugenzi wa Tfcg na mwanamtandao wakijadili jambo kuhusiana na uhifadhi wa misitu
Washiriki katika warsha
Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Mhe. Lephy Gembe akiongea kwemye warsha hiyo

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mjumita,Bi Rahima Njaidi akitoa utangulizi wa warsha ya ya siku mbili ya wadau wa mtandao huo inayoendelea Mkoani Dodoma

Mkuu wa wilaya Dodoma(suti nyeusi)akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa Mjumita