Picha: Wafanya matembezi kutoka Moshi mpaka Dar wakisafisha mazingira

Kiongozi wa msafara wa wanamazingira waliotembea kwa miguu wakiokota taka za plastiki pembezoni mwa barabara kutoka Moshi mkoani Kilima... thumbnail 1 summary
Kiongozi wa msafara wa wanamazingira waliotembea kwa miguu wakiokota taka za plastiki pembezoni mwa barabara kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro na kuja jijini Dar es Salaam, Felix Garbe (kushoto) akimkabidhi ufagio Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ubungo Kibo Dar es Salaam, Sophia Yusuf ikiwa ni ishara ya kuhamasisha wakazi wa Dar es salaam kuchukua jukumu la kutunza mazingira. Tukio hilo lilifanyika baada ya wanamazingira hao kuwasili jijini Dar es Salaam baada ya safari iliyowachukua muda wa wiki tano kumalizika.
 (Picha: Hisani ya Nipe Fagio)