MJUMITA YAPOKEA TUZO YA IKWETA

Kutoka #Paris ambapo MJUMITA Tanzania wametunukiwa tuzo ya #EquatorPrize usiku huu. Shukrani za pekee kwa WaTanzania pic.twitter.com/en... thumbnail 1 summary
Dotto Kahindi, Paris, Ufaransa
Mtandao wa Kijamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania ( MJUMITA) imepokea Tuzo ya Ikweta (Equator Prize ) kwa mwaka 2015 na kuwa kati ya Asasi 21 ambazo zimetangawa kuwa washindi wa Tuzo hiyo kwa mwaka huu.

Tuzo hiyo ya Ikweta hutolewa na Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ( UNDP) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaofadhili tuzo hiyo ambapo kila NGO iliyoshinda Tuzo hiyo imenyakua kitita cha dola 10,000 za Kimarekani sawa na milioni 21 za Kitanzania.


MJUMITA ni mtandano wenye wanachama katika vijiji 450 vilivyopo katika Wilaya 23 za Tanzania na hujishughulisha na utunzaji wa misitu, kuwasaidia wanavijiji kupata hati za kimila za kumiliki ardhi, kutatua migogoro inayohusisha masuala ya ardhi na kubuni miradi ya matumizi sahihi ya ardhi pamoja na raslimali za misitu. 
 Zaidi ya watu 500,000 wamenufaika na huduma zinazotolewa na MJUMITA, na kwamba MJUMITA ni kati ya NGO Sita kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, zilizojinyakulia tuzo hiyo. NGO nyingine zilizoshinda Tuzo Nane zinatoka Asia na Pacific na NGO nyingine Nane ni kutoka Latin Amerika na Visiwa vya Karibbean.