---------------------------------------------------------------------
Evelyn Mkokoi, Afisa Habari ofisi ya Makamu wa Rais
Evelyn Mkokoi, Afisa Habari ofisi ya Makamu wa Rais
Kibaha.
Ufuatiliaji na tathimini ya
kitaifa ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi ni njia mojawapo itakayoisaidia
Tanzania katika juhudi za pamoja za dunia za kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.
Hayo yameelezwa leo na Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula wakati wa ufunguzi wa Warsha ya
ufuatiliaji na tathmini ya kitaifa ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.
“Wote tumeshuhudia madhara
yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, yaliyojitokeza nchini kwetu ikiwa ni
pamoja na mvua kubwa zilizonyesha miaka ya hivi karibuni zilizosababisha
mafuriko, hali ya ukame, na uhaba wa chakula” alisema Salula
Salula amesema madhara yatokanayo
na mabadiliko ya tabianchi yana athiri nchi na dunia kwa ujumla lakini nchi
zilizo maskini zaidi duniani huathirika kwa kiasi kikubwa zaidi.
Alisema kuwa anaamini warsha hiyo
itasaidia kupatikamna kwa kablasha ambalo litakuwa na umuhimu kw ataifa hili
kwani litasaidia ufuatiliaji na tathmini katika suala zima la kuhimili
mabadiliko ya tabia nchi.