Alichokifanya Sean Paul kwenye utoaji wa tuzo UN wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP21, Paris, Ufaransa

Dotto Kahindi, Le Bourget, Paris, Ufaransa Disemba 10, 2015 Mwanamuziki Sean Paul alikuwa kivutio alipotumbuiza kwenye utoaji wa ... thumbnail 1 summary


Dotto Kahindi, Le Bourget, Paris, Ufaransa


Disemba 10, 2015 Mwanamuziki Sean Paul alikuwa kivutio alipotumbuiza kwenye utoaji wa tuzo za Umoja wa Mataifa kwa mashirika mbalimbali yaliyofanya vyema katika kubuni na kutekeleza shughuli za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. (Photos from Eunice Kilonzo tweets)Pamoja na kutoa vionjo vya nyimbo nyingine Sean Paul aliimba wimbo maalumu wa mabadiliko ya tabianchi unaoitwa Love Song To The Earth. 


Wimbo huo umewashirikisha wanamuziki kama Paul McCartney, Jon Bon Jovi, Sheryl Crow, Fergie, Colbie Caillat, Natasha Bedingfield, Sean Paul mwenyewe, Leona Lewis, Johnny Rzeznik, Krewella, Angelique Kidjo, Nicole Scherzinger, Kelsea Ballerini, Christina Grimmmie, Victoria Justice na Q'orianka Kilcher.